Sunday, January 19, 2014

WAKIMBIZI KATIKA BARA LA AFRIKA


Suala la wakimbizi sio suala geni kwenye vichwa vya watu wengi. Leo kama kawaida kona ya Abfafrica imeona imulike kwa kuweza kudadavua juu ya suala la wakimbizi. Kwanza kabisa kwa kutoa maana ya neno lenyewe.


 Mkimbizi ni nani?

Ni mtu au kundi la watu waliolazimika kukimbia nchi yao ili kuepuka manyanyaso, vita au vurugu. Wakimbizi huwa na hofu ya manyanyaso kutokana na rangi, dini, uraia, msimamo wa kisiasa au uanachama katika kundi fulani la kijamii. Vita na vurugu za kidini na kikabila vimekua chanzo kikuu cha wakimbizi kukimbia nchi zao.

Kuna idara maalumu iliyoanzishwa na umoja wa mataifa yenye lengo la kusimamia wakimbizi. Idara hii ni (UNHCR). Katika bara letu la Afrika nchi nyingi zenye amani zinakabiliwa na changamoto ya wakimbizi. Mfano; TANZANIA,KENYA,UGANDA,AFRIKA YA KUSINI nk. Nchi wanazotoka wakimbizi ni pamoja na Somalia, Sudan ya Kusini, Jamuhuri ya kKdemokrasia ya Kongo, Afrika ya Kati nk.  

Shirika la Umoja wa  Mataifa la Kuhudumia na Kutetea Haki za Wakimbizi

         Idara inayo shugulikia masuala ya wakimbizi (UNHCR) imeweza kutoa takwimu za idadi ya wakimbizi kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Takwimu zinaeleza kwamba watu millioni 3.1 kwa mwaka 2012 na idadi imeongezeka kwa mwaka huu wa 2014 kwakufikia watu millioni 3.4. Watu waliopotea inakadiriwa kufikia millioni 5.4 kutoka maeneo ya nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia, Sudan ya Kusini, na Mali. Vilevile watu wapatao millioni 11 wamekosa makazi. Nchini Somalia watu wanaokadiriwa millioni 2 hawana makazi na wakimbizi millioni 1 wapo maeneo ya nchi za jirani kama vile Kenya, Uganda na Tanzania. Kutoka nchini Afrika ya kati ripoti zinaonesha watu takriban 100,000 wamekimbilia nchini Cameroon  kutafuta hifadhi. 


        Mambo  yanayo sababisha wakimbizi.
  • Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaweza kuwa vya kidini, kikabila na hata uasi katika jeshi. Athari zake ni kubwa sana katika jamii. Kona ya Abfafrica imebaini asilimia kubwa ya wakina mama na watoto wanapoteza maisha kutokana na suala hili. Mfano mzuri angalia nchi ya Somalia na Sudan ya Kusini, watu na jamii zao wanakumbwa na umasikini pamoja na njaa. Pia ukosefu wa elimu unatokea hali ya kuwa uchumi unazidi kuporomoka kwa kasi kubwa. 
Wananchi wakikimbia Kongo baada ya mapigano kuzidi. Oct 2008.

  • Sababu nyingine ni umasikini na njaa unapelekea watu kukimbia nchini zao. Hebu angalia nchi ya Eritrea pamoja na Ethiopia, raia wao wanakimbilia nchi nyingine. Mfano wakati wa mashindano makubwa ya kimichezo kama vile kombe la mataifa ya Afrika, kombe la Afrika mashariki na kati, baadhi ya wachezaji ambao ni raia wa nchi hizo huwa wanatoroka katika kambi za timu zao za taifa.

  • Mapinduzi ya umwagaji damu ambayo hufanywa na wanajeshi hupelekea asilimia kubwa kukimbia nchi zao. Tuliona kipindi cha Mabutu nchini Zaire na hata Liberia, Sierra Leone, Somalia na Mali. Na hapa utasikia juu ya uvunjifu wa haki za binadamu hususani watu wanapata sana mateso kama vile kubakwa na mauaji ya kimbari. 
Baada ya kutazama vitu  hivyo, kona ya Abfafrica tukiwa kama wadau na waumini wazuri wa harakati za Afrika, tunasikititishwa sana kuona Afrika kila mwaka kunatokea matukio yanayo pelekea wakimbizi. Katika suala hili la msingi kuna vitu vinaonekana kabisa kama wa Afrika tukiamua, inawezekana vikawa historia kwa kuweza kuvikomesha mara moja. Hivi ni kwanini waasi wanazidi kushika hatamu katika bara letu? Kwani hawa hatuwajui ni akina nani na wametokea wapi? Swali hili lina jibu kabisa ndani ya vichwa vya watu wote wa bara letu hili kwa kuonesha msisitizo. Hawa waasi hawatutakii heri katika bara letu ni vibaraka tu. Hebu kwa pamoja viongozi wote wakuu wa nchi zetu za Afrika, kaeni chini mtafute njia ya kuwadhibiti hawa na wapate fundisho la milele. Waasi humaliza nguvukazi ya bara hili na hutorosha rasirimali zetu. Sisi kama wapinzani wao hebu tujitolee kuwaondoa mara moja maana ndugu zetu ambao ni wakimbizi wanapata tabu. Hebu vuta taswira na kumuangalia mama yule mjamzito na mtoto mgongoni wanavyopata tabu, halafu, je, tulitafuta uhuru wa nchi za Afrika kwaajili ya waasi? Sasa wewe kama mwana wa Afrika unasababu gani ya kuunga mkono au kuwafumbia macho waasi.

Watu walio wengi wa Afrika hatuna roho za kinyama wala za kikatili ambazo daima zinabomoa mshikamano wa nafsi na imani. Hivyo basi hatuna haja sisi kama waafrika kuwanyanyasa wala kwafukuza wakimbizi wanapokimbila katika nchi zetu kutafuta hifadhi   kwasababu tukumbuke wengi wao wanakuwa wamepoteza ndugu na jamaa zao. Hivyo hatuna budi kuwapokea na kuwasaidia kwa moyo mmoja kwa kuwapa faraja itakayo wapa matumaini katika maisha yao. Tusipo wathamini hawa ndugu zetu waafrika wenzetu,  tutamkimbilia kwa nani siku matatizo yakigeukia upande wetu. Kumbukeni ardhi ya Afrika ni mali ya waafrika. Wakoloni waliligawa bara hili kwa maslahi yao wenyewe. Hivyo hatuna budi kufuata sera za kikoloni tusiwe watu wa kuiga kutoka kwa yale mabeberu yasiyo na hata chembe ya huruma kwa binadamu wenzao. 

Ombi langu kwa umoja wa Afrika (AU) wakae chini na watathimini kwa kiwango kipi wanaweza kuwaleta waafrika pamoja. Kwa sababu ukipima kwa undani mambo yanayo tokea maeneo yenye fujo na vita kwa sauti moja yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Kikubwa hapa ni kulitazama bara la Afrika na mwenendo wake. Kipimo cha hicho ni kulileta na kulifanya bara liweze kuwa na utawala bora, uwajibikaji, usawa, haki, demokrasia ya Afrika na maadili mema kwa watu wa Afrika. Hivi ni miongoni mwa vitu ambavyo vikikosekana katika taifa fulani basi ile hali ya amani iliyokuwepo inaweza ikapotea wakati wowote. 

Kona ya abfafrica itaendelea kulisemia hili mpaka ufumbuzi wake upatikane. Vilevile tunapenda kuwashukuru wale wote wanao wasaidia hawa wakimbizi kwa kuwapa hifadhi. Sisi AFRICAN BROTHERHOOD FOUNDATION kazi yetu ni kuhakisha watu wote wa Afrika wanapata dira na mwanga katika maisha yao, na lengo kuu ni kuona Afrika inakuwa kitu kimoja na hii ndio ndoto za ndugu zetu wakimbizi pamoja na wananchi wengine wa bara hili.  Kwa ujumla wetu tukalikabili hii itatusabishia amani kurudi mara moja na kila mtu katika bara hili akajiona yupo sehemu ya salama na sauti moja ya waafrika itarudi, hii ndio kiu kubwa inayo tuandama katika jangwa hili ambalo amani yake imekuwa ikitoweka siku hadi siku. 

Waafrika sisi wenyewe tunaweza bila ya kuwezeshwa na wahisani kutoka nje. Inatupasa wenzetu wakimbizi wanavyo pata tabu na sisi tuguswe kwa namna moja ama nyingene na kwa mtazamo huu tutaweza kusaidiana kwa hatua zote tutakazo fikia. Kama ilivyo desturi yetu Afrika itajengwa na muafrika mwenyewe na kama kuibomoa tutaibomoa wenyewe. 

Narudi tena kwa hawa waasi. Hivi leo hawa jamaa wanafikiria watamuongoza nani kama wanazidi kuwaua watu wasio na hatia. Kikubwa, hawa inawezekana kabisa kuna baadhi ya serekarli zinawapa ufadhili kwasababu wana nguvu kubwa ya silaha, wamezitoa wapi? Na kwanini wanakimbilia kwenye rasirimali? Hawa wapo chini ya udhamini wa watu wasio tutakia maendeleo leo. Kwa kauli moja tunasema tena hawa ni vibaraka wa maadui wa bara la Afrika na watu wake! Shime shime viongozi wa Afrika hebu tuoneshe uzalendo kwa bara hili. Mungu ibariki Afrika!
One blood, One love, One Africa, Forever.












Saturday, January 18, 2014

JESHI LIMEFANIKIWA KUDHIBITI TENA MJI MUHIMU WA SUDAN

Bor, mji muhimu wa Sudan ya Kusini umedhibitiwa tena na wanajeshi.

wanajeshi wakifurahia ushindi katika mi wa Bor, mji ambao umebadilishwa udhibiti mara kadhaa.
Jeshi la Sudan ya Kusini limeripoti kuwa limeukamata na kudhibiti mji muhimu wa Bor kutoka kwa waasi.

Jeshi la Uganda limesema limesaidia katika oparesheni hiyo. Msemaji wa waasi anasema uamuzi wa kuondoka ulikua ni wa busara. Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei, kwa mara kadhaa umekua ukikaliwa na madaraka katika kipindi cha mwezi mmoja wa machafuko. Machafuko ambayo inaaminika yamepelekea maelfu kupoteza maisha.

Kwa wakati huo huo, mazungumzo ya kujaribu kuacha mapigano yanaendelea huko Ethiopia.

Kutokuelewana kati ya waasi na serikali kulianza tarehe 15 Disemba. Rais Salva Kiir alimshuku makamu wake wa zamani Riek Machaar kwa kujaribu kufanya mapinduzi, kitu ambacho Riek alikataa.
Mamia ya maelfu wamepoteza makazi yao wakati wa machafuko.









Bwana Kiir ni mtu wa jamii ya Dinka ambayo ni kubwa hapo nchini, wakati bwana Machar ni mtu wa jamii ya Neur. Mamia ya maelfu ya watu wamehama makazi yao katika kipindi cha machafuko.

Chanzo bbc.co.uk.

Saturday, January 11, 2014

Mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati: Wageni wasiokuwa na makazi kuondolewa.

Kambi ya muda inayohifadhi watu wanaokadiriwa kufikia 100,000 wasiokua na makazi katika uwanja wa ndege wa Mpoko, Bangui.

Awamu ya kwanza ya kuhamishwa kwa dharura kwa maelfu ya wageni waliokimbia machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imeanza leo Jumamosi.

Shirka la kimataifa la uhamiaji (IOM) limesema litaanza kuwasafirisha watu 800 wa Chad  kutoka kwenye kambi ya muda huko Bangui.

Raisi wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michael Djotodia alijiuzulu Ijumaa kutokana na maigano kati ya wapiganaji wa kiislam na kikristo.



Bwana Djotodia, raisi wa kwanza muislam, aliyepata madaraka mwaka uliopita. Toka hapo 20% ya watu wamelazimika kukimbia ili kuepuka vurugu.

Watu wasiopungua 1,000 wamefariki toka machafuko yaanze mwezi December.

Kwa sasa umoja wa Afrika ina watunza amani 4,000 ndani ya nchi. Sambamba na hilo Ufaransa inapeleka vikosi 1,600 kwenda kujaribu kurejesha amani.



Kiongozi wa umoja wa mataifa ametoa tahadhari ya kutokea majanga makubwa ya kiubinadamu.

Bofya hapa kwa taarifa zaidi.

Chanzo BBC.

Mgogoro wa Sudani ya Kusini: UN yatoa wito kwa serikali kuwaachia wafungwa

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limemuomba rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir awaachie wafungwa wa kisiasa ili kusaidia katika kuhitimisha machafuko yanayoendelea. 



Kiongozi wa waasi, Riek Machar, anataka watu kumi na moja waachiwe huru kabla ya makubaliano ya amani kufanyika.

Vikosi vya Machaar vinaonekana kuzidiwa nguvu baada ya kupoteza mji wa Bentiu na kuchukuliwa na majeshi ya serikali katika siku ya Ijumaa.

Serikali inasema inapeleka maelfu ya vikosi ili kudhibiti Bor - mji mkubwa na wa mwisho unaodhibitiwa na vikosi vya waasi.

Machaar, makamu wa raisi aliyefukuzwa kazi, ameonesha nia ya kuendelea kudhibiti mji huo ambao upo umbali wa km 200 kaskazini mwa mji mkuu wa Juba.



Akiongea na AFP kwa simu, wakala wa habari, aliyejaribu kueleza tukio la waasi kupoteza mji huo:
"Ilikua ni kuepuka mapigano katika mitaa na kulinda maisha ya raia," alisema.

Msemaji wa jeshi  Philip Aguer amesema baadhi ya wapiganaji wa pande zoe wamepoteza maisha.

Pamoja na serikali kuingia katika mji huo, maelfu ya watu wameihama Bentiu, na maelfu kadhaa ya watu wametafuta hifadhi katika kambi ya UN hapo mjini.

Kwa taarifa zaidi endelea hapa.

Chanzo www.bbc.co.uk/news

Vikosi vya Sudani ya kusini vimefanikiwa tena kudhibiti mji muhimu wa Bentiu.

Andrew Harding wa BBC ameripoti kuwa ineonakana Bentiu ilidhibitiwa kutoka kwa waasi kukiwa na "upinzani mdogo tu."

 Jeshi la Sudani ya Kusini linasema wamefanikiwa kudhibiti tena kitovu cha mafuta Bentiu, mji ambao ni moja ya miji miwili tu inayoshikiliwa na waasi.


Msemaji wa jeshi Philip Aguer kipingamizi cha mwisho ambacho  kilikua ni kifaru kilichokua kinalinda daraja la kuingia katika mji huo. Hata hivyo walifanikiwa kukidhibiti saa 14:30 kwa majira ya huko.

Kiongozi wa waasi Riek Machar ameiambia AFP kuwa vikosi vyake vimeondoka ili tu kutunza amani kwa wananchi ila wameapa kuendeleza mapigano.

Mkuu wa kutunza amani wa UN anasema machafuko hayo yameua watu wasiopungua 1,000.

Mazungumzo ya kutuliza mapigano katika mji wa jirani huko Ethiopia yamesimama.


Endelea hapa kwa taarifa zaidi.

Chanzo www.bbc.co.uk

Friday, January 10, 2014

RAISI WA MPITO WA JAMHURI YA AFRICA YA KATI AJIUZULU


Michel Djotodia rahisi wa mpito wa CAR

Raisi wa mpito wa jamhuri ya Afrika ya kati Michael Djotodia amejiuzulu katika mkutano wa kilele uliokua na lengo la kumaliza mapigano ambayo yameikumba nchi..

Mkutano wote wa mpito unahudhuri mkutano huko Chad ulioitishwa na Wakuu wa nchi.

Michael Djotodia ni rais wa kwanza muislam wa Jamhuri wa Afrika ya Kati aliyepata madaraka mwaka jana.

Toka Disemba na kuwasili zaidi kwa watunza amani na vikosi vya Ufaransa, 
watu 1,000 wamepoteza maisha katika mapigano ya kiitikadi.

Vitongoji vingi vimeteketezwa na mwishoni mwa mwezi uliopita idadi ya watu ambao wamekimbia makazi ya imeongezeka kwa mara mbili ukihisha karibia nusu ya wale ambao wanaishi katika mji mkuu wa Bangui.

Kumekua na matukio ya furaha kwa watu baada ya kutolewa tangazo hilo huko Chad.

Carine Gbegbe, ambaye amekua akiishi katika kambi ya watu wasiokua na makazi, amekiambia chanzo husika, "Hatimaye tupo huru. Tunaelekea kurudi nyumbani".

Vifaru vya Ufaransa haraka vilipelekwa ikulu.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesisitiza mbadala kwa bw. Djotodia ufanyike "haraka iwezekanavyo".



Tuesday, January 7, 2014

UMASIKINI NA NJAA NDANI YA AFRIKA YETU.

       Katika hali isio ya kawaida watu wengi tunajiuliza maswali mengi kama haya;
i) Kwanini Afrika ni masikini?
ii) Inawezekana vipi A­­­­­frika kuwa masikini huku ina rasilimali za kutosha?
iii) Mbona viongozi wengi wa Afrika wana hodhi mali nyingi ugaibuni hali ya kuwa watu wanaowaongoza ni masikini?.

Haya ni baadhi ya maswali kati ya mengi ambayo watu hujiuliza katika vichwa vyao. Kona ya Abfafrica, inataka leo ijikite kwenye suala hili ilikuweza kupatia ufumbuzi wa haya masuala yanayo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Tafsiri ya umasikini ina uwanja mpana katika fikra za watu mbalimbali hususani waliokuwa bobezi katika masuala ya lugha hii adhimu ya kiswahili.

Umasikini ni hali ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu au ya lazima kwa lugha nyingine kama vile chakula, maji masafi, huduma bora za afya, mavazi na hata nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvipata au kununua kwa ukosefu wa kipato.

Kona ya Abfafrica haina lengo la kulaumu kama ilivyo desturi ya watu walio wengi bali ina madhumuni ya kuelimisha jamii kama ilivyo desturi yetu waAfrika, ili kuweza kuondokana na vikwazo hivi vikubwa vya kimaisha.

Ukipitia vyanzo mbalimbali vya habari kuna takwimu zimetolewa na shirika la chakula duniani maarufu kama (FAO) zinaonesha kwa jinsi gani bara la Afrika linavyokumbwa ya watu wenye njaa na umasikini. Kwa upande wetu wa Afrika idadi imeongezeka kutoka watu millioni 175 hadi millioni 239, vilevile idadi ya watu millioni 20 iliongezeka huku takwimu ikionesha asilimia 2% inaongezeka kila mwaka hii ni taarifa ya mwaka (2012).

Njaa na umasikini ni vitu ambavyo vinashabihiana kwa kua umasikini huleta njaa na njaa vilevile huleta umasikini.

Kona ya Abfafrica imebaini sababu za umasikini na njaa, ukosefu wa uchumi imara ambao unapelekea wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wa Afrika imekuwa ni wimbo wa taifa kwao vilevile hupelekea bara la Afrika kuwa tegemezi kwa mataifa ya magharibi.

Matokeo ya hili ni serikali nyingi za Afrika zinakutana na mashariti makubwa na umasikini unazidi kushika kasi, vilevile vita vya wenyewe kwa wenyewe ndio chanzo kingine cha njaa na umasikini kwa kua watu wanakosa muda wa kuzalisha. Akina mama na watoto ndio wanaathirika kwa kiwango cha juu na hupelekea miji kuwa magofu, idadi ya watu inapungua kutokana na vifo vinaongezeka.


Angalia ndugu zetu wa Sudan ya kusini wanavyo pata shida, ukosefu wa miundombinu katika nchi za Afrika sehemu kubwa ya maeneo ya vijiji katika bara hili hakuna huduma nzuri za barabara za kiwango cha lami, uhaba wa reli na hata vivuko imara angalia mfano wa nchi kama Mali, Burkina Fasso, Sudani ya kusini, Jamuhuri ya Watu wa Afrika ya kati, DRC kongo, Tanzania nk, watu wanapata shida za usafiri na mawasiliano ambayo ni katika vyanzo vikuu vya kiunua kwa haraka uchumi ndio maana tunazidi kuwa masikini wa kupindukia. Mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira inapelekea maeneo mengi ya Afrika kukumbwa na njaa pamoja na umasikini usio malizika.

Imeandaliwa na kona ya Afrcan Brotherhood Foundation.

One Blood, One Love, One Africa forever!!!