Kuhusu sisi

AFRICAN BROTHERHOOD FOUNDATION (ABF)
        Taasisi hii inawalenga watu wote wa bara la afrika. Ina malengo ya kuwaunganisha waafrika katika nyanja za kiuchumi,kijamii na hata kisiasa ili kulifanya bara la Afrika kupata maendeleo endelevu na kuweza kujitegemea katika masuala yake mbalimbali. Taasisi hii imeanzishwa 15-12-2013 na muasisi ni FARIDI FARAJI. 
Malengo ya taasisi hii ni haya yafuatayo.

(i) Kuwaunganisha waafrika kiuchumi yaani tuweze kutumi fedha ya aina moja na                       kuanzishwa benki ya afrika ambayo itaendeshwa kwa mfumo wa kiafrika yaani bila                     matumizi ya riba,

(ii) Kutumia lugha moja yaani kiswahili kama lugha ya mawasiliano ya bara zima na                     vilevile taasisi itakuwa ina toa elimu kwa njia mbalimbali kama vipeperushi,semina na                 hata kuwatembelea wagonjwa watoto yatima na wafungwa katika bara la afrika.

(iii) Kupigania usawa na kutetea haki za waafrika duniani kote.

       (iv) Kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unapatikana kwa watu wote wa bara la afrika.

(v) Kusisitiza uadilifu na kuwatetea viongozi wetu wa afrika kwa nguvu moja.

(vi) Kupatikana kwa ufanisi na demokrasia ya afrika ambayo itaweza kuleta tija na                       upendo kwa watu wa afrika.

(vii) Kupigania na kutetea rasilimali za waafrika zisimamiwe na watu waafrika wenyewe.

(viii) Kufanikisha kupatikana kwa jamuhuri ya muungano ya watu wa Afrika.

No comments:

Post a Comment