Katika hali
isio ya kawaida watu wengi tunajiuliza maswali mengi kama haya;
i) Kwanini Afrika ni
masikini?
ii) Inawezekana vipi Afrika
kuwa masikini huku ina rasilimali za kutosha?
iii) Mbona viongozi wengi
wa Afrika wana hodhi mali nyingi ugaibuni hali ya kuwa watu wanaowaongoza ni
masikini?.
Haya ni
baadhi ya maswali kati ya mengi ambayo watu hujiuliza katika vichwa vyao. Kona
ya Abfafrica, inataka leo ijikite kwenye suala hili ilikuweza kupatia ufumbuzi
wa haya masuala yanayo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Tafsiri ya
umasikini ina uwanja mpana katika fikra za watu mbalimbali hususani waliokuwa
bobezi katika masuala ya lugha hii adhimu ya kiswahili.
Umasikini ni
hali ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu au ya lazima kwa lugha nyingine
kama vile chakula, maji masafi, huduma bora za afya, mavazi na hata nyumba
kutokana na kukosa uwezo wa kuvipata au kununua kwa ukosefu wa kipato.
Kona ya Abfafrica
haina lengo la kulaumu kama ilivyo desturi ya watu walio wengi bali ina
madhumuni ya kuelimisha jamii kama ilivyo desturi yetu waAfrika, ili kuweza
kuondokana na vikwazo hivi vikubwa vya kimaisha.
Ukipitia
vyanzo mbalimbali vya habari kuna takwimu zimetolewa na shirika la chakula
duniani maarufu kama (FAO) zinaonesha kwa jinsi gani bara la Afrika
linavyokumbwa ya watu wenye njaa na umasikini. Kwa upande wetu wa Afrika idadi
imeongezeka kutoka watu millioni 175 hadi millioni 239, vilevile idadi ya watu
millioni 20 iliongezeka huku takwimu ikionesha asilimia 2% inaongezeka kila
mwaka hii ni taarifa ya mwaka (2012).
Njaa na
umasikini ni vitu ambavyo vinashabihiana kwa kua umasikini huleta njaa na njaa
vilevile huleta umasikini.
Kona ya
Abfafrica imebaini sababu za umasikini na njaa, ukosefu wa uchumi imara ambao
unapelekea wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wa Afrika
imekuwa ni wimbo wa taifa kwao vilevile hupelekea bara la Afrika kuwa tegemezi
kwa mataifa ya magharibi.
Matokeo ya
hili ni serikali nyingi za Afrika zinakutana na mashariti makubwa na umasikini
unazidi kushika kasi, vilevile vita vya wenyewe kwa wenyewe ndio chanzo kingine
cha njaa na umasikini kwa kua watu wanakosa muda wa kuzalisha. Akina mama na
watoto ndio wanaathirika kwa kiwango cha juu na hupelekea miji kuwa magofu,
idadi ya watu inapungua kutokana na vifo vinaongezeka.
Angalia
ndugu zetu wa Sudan ya kusini wanavyo pata shida, ukosefu wa miundombinu katika
nchi za Afrika sehemu kubwa ya maeneo ya vijiji katika bara hili hakuna huduma
nzuri za barabara za kiwango cha lami, uhaba wa reli na hata vivuko imara
angalia mfano wa nchi kama Mali, Burkina Fasso, Sudani ya kusini, Jamuhuri ya
Watu wa Afrika ya kati, DRC kongo, Tanzania nk, watu wanapata shida za usafiri
na mawasiliano ambayo ni katika vyanzo vikuu vya kiunua kwa haraka uchumi ndio
maana tunazidi kuwa masikini wa kupindukia. Mabadiliko ya tabia nchi na
uharibifu wa mazingira inapelekea maeneo mengi ya Afrika kukumbwa na njaa
pamoja na umasikini usio malizika.
Imeandaliwa na kona ya Afrcan Brotherhood Foundation.
One Blood, One Love, One Africa forever!!!