Tuesday, January 7, 2014

UMASIKINI NA NJAA NDANI YA AFRIKA YETU.

       Katika hali isio ya kawaida watu wengi tunajiuliza maswali mengi kama haya;
i) Kwanini Afrika ni masikini?
ii) Inawezekana vipi A­­­­­frika kuwa masikini huku ina rasilimali za kutosha?
iii) Mbona viongozi wengi wa Afrika wana hodhi mali nyingi ugaibuni hali ya kuwa watu wanaowaongoza ni masikini?.

Haya ni baadhi ya maswali kati ya mengi ambayo watu hujiuliza katika vichwa vyao. Kona ya Abfafrica, inataka leo ijikite kwenye suala hili ilikuweza kupatia ufumbuzi wa haya masuala yanayo tukabili katika maisha yetu ya kila siku. Tafsiri ya umasikini ina uwanja mpana katika fikra za watu mbalimbali hususani waliokuwa bobezi katika masuala ya lugha hii adhimu ya kiswahili.

Umasikini ni hali ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya binadamu au ya lazima kwa lugha nyingine kama vile chakula, maji masafi, huduma bora za afya, mavazi na hata nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvipata au kununua kwa ukosefu wa kipato.

Kona ya Abfafrica haina lengo la kulaumu kama ilivyo desturi ya watu walio wengi bali ina madhumuni ya kuelimisha jamii kama ilivyo desturi yetu waAfrika, ili kuweza kuondokana na vikwazo hivi vikubwa vya kimaisha.

Ukipitia vyanzo mbalimbali vya habari kuna takwimu zimetolewa na shirika la chakula duniani maarufu kama (FAO) zinaonesha kwa jinsi gani bara la Afrika linavyokumbwa ya watu wenye njaa na umasikini. Kwa upande wetu wa Afrika idadi imeongezeka kutoka watu millioni 175 hadi millioni 239, vilevile idadi ya watu millioni 20 iliongezeka huku takwimu ikionesha asilimia 2% inaongezeka kila mwaka hii ni taarifa ya mwaka (2012).

Njaa na umasikini ni vitu ambavyo vinashabihiana kwa kua umasikini huleta njaa na njaa vilevile huleta umasikini.

Kona ya Abfafrica imebaini sababu za umasikini na njaa, ukosefu wa uchumi imara ambao unapelekea wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wa Afrika imekuwa ni wimbo wa taifa kwao vilevile hupelekea bara la Afrika kuwa tegemezi kwa mataifa ya magharibi.

Matokeo ya hili ni serikali nyingi za Afrika zinakutana na mashariti makubwa na umasikini unazidi kushika kasi, vilevile vita vya wenyewe kwa wenyewe ndio chanzo kingine cha njaa na umasikini kwa kua watu wanakosa muda wa kuzalisha. Akina mama na watoto ndio wanaathirika kwa kiwango cha juu na hupelekea miji kuwa magofu, idadi ya watu inapungua kutokana na vifo vinaongezeka.


Angalia ndugu zetu wa Sudan ya kusini wanavyo pata shida, ukosefu wa miundombinu katika nchi za Afrika sehemu kubwa ya maeneo ya vijiji katika bara hili hakuna huduma nzuri za barabara za kiwango cha lami, uhaba wa reli na hata vivuko imara angalia mfano wa nchi kama Mali, Burkina Fasso, Sudani ya kusini, Jamuhuri ya Watu wa Afrika ya kati, DRC kongo, Tanzania nk, watu wanapata shida za usafiri na mawasiliano ambayo ni katika vyanzo vikuu vya kiunua kwa haraka uchumi ndio maana tunazidi kuwa masikini wa kupindukia. Mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira inapelekea maeneo mengi ya Afrika kukumbwa na njaa pamoja na umasikini usio malizika.

Imeandaliwa na kona ya Afrcan Brotherhood Foundation.

One Blood, One Love, One Africa forever!!!

No comments:

Post a Comment