Saturday, January 18, 2014

JESHI LIMEFANIKIWA KUDHIBITI TENA MJI MUHIMU WA SUDAN

Bor, mji muhimu wa Sudan ya Kusini umedhibitiwa tena na wanajeshi.

wanajeshi wakifurahia ushindi katika mi wa Bor, mji ambao umebadilishwa udhibiti mara kadhaa.
Jeshi la Sudan ya Kusini limeripoti kuwa limeukamata na kudhibiti mji muhimu wa Bor kutoka kwa waasi.

Jeshi la Uganda limesema limesaidia katika oparesheni hiyo. Msemaji wa waasi anasema uamuzi wa kuondoka ulikua ni wa busara. Bor, mji mkuu wa jimbo la Jonglei, kwa mara kadhaa umekua ukikaliwa na madaraka katika kipindi cha mwezi mmoja wa machafuko. Machafuko ambayo inaaminika yamepelekea maelfu kupoteza maisha.

Kwa wakati huo huo, mazungumzo ya kujaribu kuacha mapigano yanaendelea huko Ethiopia.

Kutokuelewana kati ya waasi na serikali kulianza tarehe 15 Disemba. Rais Salva Kiir alimshuku makamu wake wa zamani Riek Machaar kwa kujaribu kufanya mapinduzi, kitu ambacho Riek alikataa.
Mamia ya maelfu wamepoteza makazi yao wakati wa machafuko.









Bwana Kiir ni mtu wa jamii ya Dinka ambayo ni kubwa hapo nchini, wakati bwana Machar ni mtu wa jamii ya Neur. Mamia ya maelfu ya watu wamehama makazi yao katika kipindi cha machafuko.

Chanzo bbc.co.uk.

No comments:

Post a Comment